Mbowe akamatwa mjini Dar es Salaam.

Freeman Mbowe Haki miliki ya picha ippmedia
Image caption Freeman Mbowe

Nchini Tanzania kiongozi wa chama kikuu cha upinzani, Chadema, amekamatwa mjini Dar es Salaam.

Freeman Mbowe anakabili mashtaka ya kufanya mkutano bila ya ruhusa, na fujo, kuhusu maandamano yaliyofanywa mapema mwaka huu.

Kiongozi mwengine wa upinzani, Zitto Kabwe, ambaye ni naibu katibu mkuu wa Chadema, alizuwiliwa na polisi kwa muda mfupi, hapo jana, na kuachiliwa kwa dhamana.