Jol ndiye kocha mpya wa Fulham

Timu ya Fulham inayocheza katika ligi kuu ya England imemteua Martin Jol kama kocha mpya wa timu hiyo kufwatia kujiuzulu kwa Mark Hughes wiki iliopita.

Image caption Kocha mpya wa Fulham Martin Jol

Kocha huyo wa zamani wa Tottenham na Ajax anajiunga na klabu ya England ya premia kwa mkataba wa awali wa miaka miwili,atakuwa na fursa ya kuongeza mwaka mmoja tena.

Jol amesema: "Nina furaha sana kujiunga na Fulham.Ni timu yenye msingi imara na mashabiki wa dhati.

"Natarajia kuwa sehemu ya jamii ya Fulham na namshukuru mwenyekiti kwa kuniamini."

Hughes aliondoka katika nafasi yake ya kocha wa Fulham tarehe 2 Juni na amekuwa huko kwa chini ya mwaka mmoja.

Alijiunga na Fulham mwezi Julai 2010 na amekuwa katika mashauriano juu ya kupewa kandarasi mpya kabla ya kujiuzulu.

Jol alijiunga na spurs mwaka 2004 kama kocha msaidizi wa Jacques Santini lakini akawa kocha mkuu mwezi Novemba 2004 baada ya Santini kujiuzulu.