Mashambulizi ya Boko Haramu

Takriban watu watano wameuawa baada ya vituo vya polisi kushambuliwa katika mji wa Maiduguri ulioko kaskazini mwa Nigeria taarifa za hospitali zimesema.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mandhari ya Maiduguri

Mwandishi wa BBC Bilkisu Babangida aliyeko katika mji huo anasema kulikuwa na milipuko mitatu na milio ya risasi ilisikika katika kil kinachoaminika kuwa ni shambulio la kikundi cha Boko Haram.

Wafuasi wa kundi hilo Boko Haramu wameua maofisa wengi wa polisi pamoja na wanasiasa katika mji huo katika kiinmdi cha mwaka mmoja uliopita.

Lengo lake ni kuipindua serikali ya Nigeria kwa imani kuwa elimu kutoka magharibi ni mbovu.

Mnamo mwaka 2009 maelfu wa wafuasi wa kundi hili waliuawa huko Maiduguri baada ya kushambulia vituo kadhaa vya polisi.

Mashambulizi ya hivi karibuni yanatokea siku moja baada ya madai kwamba kundi hilo lilimua Imamu mmoja kutoka madhehebu wasiokubaliana na imani yao kwa kuwakosoa.

Ibrahim Birkuti aliuawa kwa risasi akiwa nyumbani kwake katika mji wa Biu ulio umbali wa kilomita 200 kusini mwa mji wa Maiduguri.

Kama wenzake waliomtangulia aliyemuua alikuwa juu ya pikipiki.

Image caption maiti zapangwa juu ya gari

Wiki iliyopita kundi hili la Boko Haram liliiambia BBC kuwa lilipanga mfululizo wa milipuko kufuatia kuapishwa kwa Rais Goodluck Jonathan.

Msemaji wake alisema kuwa wao ndiyo waliomuua kakake Shehu wa Borno, mmojapo wa viongozi muhimu wa Kiislamu nchini Nigeria.

Polisi wamekamata maelfu ya watu na vilevile kupiga marufu safari za pikipiki nyakati za usiku ila hayo hayajaweza kukomesha ghasia hizi.