Sudan haikuruhusu mauaji ya Abyei- UN

Ban Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ban Ki-moon asema hakuna ushahidi Sudan kuruhusu mauaji Abyei

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon amekatalia mbali madai kuwa wakuu wa serikali nchini Sudan wameruhusu mauaji ya kikabila katika jimbo linalozozaniwa la Abyei.

Amewaambia waandishi wa habari kuwa hakuna ushahidi unaoonyesha kuwepo kwa kampeni hiyo.

Maelfu ya watu kutoka Sudan Kusini wamekimbia Abyei tangu wanajeshi kutoka kaskazini walipoingia eneo hilo mwezi uliopita.

Bwana Ban amesema serikali ya Sudan imeashiria kuwa itawaruhusu watu hao kurejea Abyei.

Sudan Kusini inatazamiwa kutangazwa kuwa taifa huru mwezi ujao.