US:Yemen ifanye mabadiliko mara moja

Waandamanaji Yemen Haki miliki ya picha AP
Image caption Waandamanaji Yemen

Marekani kwa mara nyingine imetowa wito wa kudalishana madaraka mara moja nchini Yemen.

Hii ni baada ya rais wa taifa hilo Ali Abdullah Saleh kuondoka nchini humo, kwa matibabu nchini Saudi Arabia.

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Hillary Clinton amesema ni hatua kama hiyo tu ndio itakayokuwa na manufaa kwa watu wa Yemen.

Rais Saleh yuko nchini Saudi Arabia kufanyiwa matibabu baada ya kujeruhiwa katika shambulio la kombora wiki iliyopita.

Wakati huo huo duru nchini Uingereza zinaarifu kuwa wanajeshi wa taifa hilo wako chonjo katika pwani ya Yemen kuwasaidia raia wa Uingereza kuondoka nchini humo ikiwa itabidi.

Maafisa wanane wa jeshi la wanamaji kutoka Uingereza wameripotiwa kuabiri meli ya kivita inayoshika doria katika pwani ya Yemen.