Bajeti za Afrika Mashariki zasomwa

Image caption Serikali imetangaza hatua ya kudhibiti bei ya chakula

Kenya imetangaza bajeti inayolenga kukabiliana na ongezeko la gharama ya maisha na kudhibiti bei ya bidhaa nchini humo.

Waziri wa fedha Uhuru Kenyatta katika taarifa yake ya makadirio ya matumizi ya mwaka 2011/2012 amesema serikali itaondoa ushuru wa mafutaa ya taa.

Serikali ya pia imetangaza hatua ya kuwaondolea waagizaji mahindi na ngano ushuru . Hii ina lengo la kukabiliana na upungufu unga wa mahindi na ngano nchini Kenya uliosababishwa na mazao duni kutokana na ukame

Hata hivyo bei ya sigara na pombe inatarajiwa kupanda kwani ushuru wake umeongezwa.

Katika kuwasaidia akina mama wajawazito wanaoishi mashambani ili waweze kufika hospitalini kwa wasaa ,ushuru kwa wanaotaka kuagiza magari ya wagonjwa na pikipiki umeondolewa.

Serikali ya Kenya pia imetenga pesa zaidi za kununua dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi ili watu wanaoishi na virusi hivyo waweze kunufaika.

Uganda

Haki miliki ya picha weinformers.net
Image caption Maria Kiwanuka

Na kutoka Uganda,Mwandishi wetu Alli Mutasa anaripoti kuwa katika bajeti yake ,Uganda ina lengo la kuikuza nchi hiyo kiuchumi , kubuni ajira na kuimarisha utoaji wa huduma.

Lakini kufanikisha hayo yote Uganda inatarajia kukusanya dola bilioni 2.5 kutoka ndani ya nchi hii ikiwa ni asilimia 66 .

Waziri mpya wa Fedha wa Uganda ,Bi Maria Kiwanuka, anasema ili nchi hiyo iweze kufanikisha malengo yake itategemea kwa kiwango kikubwa nchi wafadhili ili kuweza kujaliza pengo la asilimia 24 katika bajeti yake.

Huku Uganda ikitarajia kupata ufadhili kutoka nchi marafiki , bado nchi hiyo inazongwa na deni la zaidi ya dola bilioni 4.