Mzozo wa Abyei kujadiliwa Adis Ababa

Rais wa Sudan Kusini Salva Kirr Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Sudan Kusini Salva Kirr

Viongozi wa Sudan Kusini na Kaskazini wanajadiliana mpango wa kuondoa wanajeshi katika eneo la mpakani linalozozaniwa la Abyei, huku ikiwa imesalia mwezi mmoja tu, kabla ya eneo la Sudan Kusini kujinyakulia uhuru wake.

Muungano wa Afrika, ambao unaandaa mkutano huo mjini Adis Ababa, Ethiopia, umependekeza wanajeshi wa kutunza amani wa muungano huo, kutumwa katika eneo hilo, ili kuruhusu raia waliokimbia makwao kurejea.

Rais wa Sudan Omar Al Bashir na mwenzake wa Sudan Kusini, Salva Kirr wanahudhuria mkutano huo.

Ripoti ambazo hazijathibitisha zinasema pande hizo mbili zinakaribia kuafikiana.