Domenech huenda akateuliwa kocha wa Algeria

Aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa, Raymond Domenech amesema angependa kuwa kocha wa Algeria, baada ya kushauriwa kuchukua wadhifa huo.

Image caption Aliyekuwa kocha wa Ufaransa Raymond Domenech

Nafasi hiyo ya kocha wa timu ya Desert Foxes pia inawaniwa na aliyekuwa kocha wa Ivory Coast Vahid Halilhozdic.

Kocha wa timu hiyo Abdelhak Benchikha alijiuzulu mapema mwezi huu baada ya timu hiyo kushindwa na Morocco katika mechi ya kufuzu kwa kombe la taifa bingwa barani Afrika mjini Casablanca.

Washauri wanasema kocha huyo ameombwa na maafisa wa shirikisho la soka nchini Algeria kukubali wadhifa huo.

Ripoti zinasema Halilhozdic anatarajiwa kushauriana na wakuu wa shirikisho la soka nchini Algeria siku ya Ijumaa kujadili wadhifa huo mjini Paris.

Domenech,ambaye alimrithi Jacques Santini mwaka wa 2004, baada ya matokeo duni ya timu hiyo ya Ufaransa katika fainali za kombe la dunia, ambapo Ufaransa iliondolewa katika raundi ya kwanza.

Image caption Mashabiki wa timu ya Algeria

Mwaka wa 2006 aliongoza Ufaransa kufika fainali hizo za kombe la dunia, ambapo walishindwa kwenye fainali na Italia kwa njia ya penalti, baada ya Zinedine Zidane kupewa kadi nyekundu dakika za ziada kipindi cha pili.

Aliyekuwa mlinzi wa Manchester United Laurent Blanc alimrithi Domenech julai mwaka huu na kuongoza Ufaransa katika kundi lao ya michuano ya kufuzu kwa michuano ya kombe la taifa bingwa barani ulaya mwaka ujao.

Benchikha alijiuzlu kama kocha wa Algeria baada ya kunyukwa mabao 4-0 na Morocco.

Algeria sasa inashikilia nafasi ya mwisho katika kundi D, Morocco ikiwa ya kwanza ikifuatwa na Jamuhuri ya Afrika ya Kati na Tanzania.