Mke wa mwanabalozi wa DRC akamatwa

Mke wa mwanabalozi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo amekamatwa nchini Romania kwa tuhuma za kuendesha biashara ya magendo ya sigara.

Polisi imekamata zaidi ya pakiti za sigara 18,000 zilizofichwa ndani ya gari lake.

Image caption Biashara ya magendo

Bi.Esther Pascaline Bombeto, ambaye mume wake anafanya kazi kwenye ubalozi wa nchi yake nchini Serbia, imearifiwa kwamba alidai kuwa gari lake haliwezi kuchunguzwa kutokana na hadhi yake kibalozi lakini polisi wakavunja gari lake. Bibi huyo alikuwa njiani kutoka Serbia alipokamatwa.

Madirisha yalivunjwa na maofisa wa idara ya ujasusi wakishirikiana na polisi wanaopambana na uhalifu.

Hadi kusaka gari hilo walimfuatilia kwa miezi kadhaa na kuhakiki kuwa kweli anasafirisha biashara ya sigara na kuivusha mpaka.

Kwa kutumia kibali cha mwanadiplomasia, waendesha biashara hiyo ya magendo walisafirisha sigara zao kutoka Serbia hadi Romania mara mbili kwa kila wiki, alisema mwendesha mashtaka wa uhalifu uliopangwa Mircea Andres.

Image caption Hupatikana sokoni

Maofisa walivunja madirisha ya gari la Bi Bombeto na kukamata sigara zilizotengenezwa huko Albania ambazo walidai baada ya yeye binafsi kukataa kushirikiana nao.

Raia wawili wa Serbia wanaodaiwa kuwa washirika wa Bi Bombeto wamekamatwa pia.

Wakati huo huo polisi walikuwa wakipeleleza nyumba tisa za washukiwa wengine walioshiriki biashara hiyo nchini Romania.