Sudan ya kusini yaomba msaada UN

Katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja Sudan ya kusini inatarajiwa kuwa Taifa huru ikijikwamua kutoka Sudan ya kaskazini.

Haki miliki ya picha 1
Image caption Sudan bado mashakani

Kordofan ya kusini itabaki kuwa chini ya uangalizi wa Sudan ya kaskazini lakini kufuatia mapigano ya hivi karibuni pamoja na mashambulio ya anga takriban watu elfu sitini wamesambaratishwa.

Umoja wa Mataifa umeishutumu serikali ya Sudan kwa 'kampeni kali ya kudondosha mabomu' karibu na mpaka baina ya kaskazini na kusini.

Mashirika ya kutowa misaada yanasema kuwa maelfu ya watu wamekimbia kutoka nyumba zao, na kuitaka serikali ya Kaskazini iyaruhusu mashirika yaweze kupita ili kuwasaidia watu hao.

Haki miliki ya picha AP
Image caption kujitenga karibuni

Naibu wa Rais wa Sudan ya kusini, Riek Machar ameomba Umoja wa Mataifa usaidie katika kuhifadhi amani katika eneo hilo.

Bwana Machar ameisihi serikali ya Sudan ya kaskazini isikilize sauti ya jumuia ya kimataifa ya kuitaka iondoke Abyei.