McLeish kuteuliwa kocha wa Aston Villa

BBC imegundua kuwa klabu cha Aston Villa kitatamngaza rasmi kocha wake mpya baada ya mazungumzo kati ya wasimamizi wa klabu hicho na Alex McLeish.

Haki miliki ya picha Other
Image caption Kocha wa zamani wa Klabu cha Birmingham

Mmiliki wa Aston Villa, Randy Lerner na McLeish wameafikiana kuhusu wadhifa huo.

McLeish alijiuzulu kama kocha wa klabu cha Birmingham City siku ya Jumapili.

Takriban, mashabiki 500 walikusanyika nje ya uwanja wa nyumbani wa klabu hiyo wa Villa Park kupinga uwezekano wa kuteuliwa kwa raia huyo wa Uskochi kama kocha wao mpya.

Image caption Wachezaji wa Aston Villa wakisherekea kufunga bao

McLeish alisitisha likizo yake mjini Corsica na kurejea nchini Uingereza ili kushauriana na Lerner hapo jana.

Siku ya Jumanne, Villa, ilisema kuwa, wanafahamu kuwa kocha huyo hana uhusiano na klabu chochote na kwamba wana nia ya kumsaili, kuhusu uwezekano wa kuchukua wadhifa huo.

Lakini klabu cha Birmingham kimetoa taarifa ikiwashutumu majirani wao kwa kuawapokonya kocha.