Ugiriki yaweza kushindwa kulipa madeni

George Papandreou anasheherekea mwaka wake wa 59 kwa umri, na zawadi alioipokea ni kujiuzulu kwa manaibu wawili wa mawaziri katika chama cha kisoshalisti.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Waziri mkuu wa Ugiriki

Wakati waasi hao wakimuacha mkono, Rais Karolos Papoulias ametaka pawepo na uwajibikaji ili mgogoro wa uchumi usigeuzwe kuwa medani ya kisiasa.

Hali hiyo ya sintofahamu imemtia wasiwasi kamishena wa fedha wa Umoja wa Ulaya Olli Rehn ambaye azma yake ni kuona kwamba sarafu ya Euro haitoathiriwa na mgogoro wa hivi sasa.

Amezitaka serikali za umoja huo zipuuze tofauti zao wakati huu mgumu na zikubaliane juu ya fungu la kuiokoa Ugiriki kwa mara ya pili kufikia mwezi Julai.

Huu ni mwezi muhimu kwa Ugiriki ambayo ina pesa kidogo na itaishiwa mnamo mwezi huo ikiwa haitopokea kitita cha kwanza kama ilivyoahidiwa mnamo mwezi Mei mwaka 2010.