Sharaf apendekeza uchaguzi wa bunge kuahirishwa

Essam Sharaf
Image caption Essam Sharaf

Waziri Mkuu wa Misri, Essam Sharaf, alisema anapendelea uchaguzi wa bunge kuahirishwa ili vyama vipya vya kisiasa vipate muda zaidi kujitayarisha.

Bwana Sharaf piya aliunga mkono kampeni inayoendelea kutaka katiba mpya itungwe kabla ya uchaguzi.

Halmashauri ya kijeshi iliyochukua madaraka, baada ya Rais Mubarak kuondolewa kutokana na maandamano ya mwezi Februari, imepanga uchaguzi kufanywa mwezi wa Septemba na ufwatiwe na uchaguzi wa rais baada ya mwaka mmoja.