Wabeba vikombozi wafungwa

Haramia Somalia Haki miliki ya picha elvis
Image caption Haramia Somalia

Mahakama ya Somalia yameamua kifungo cha miaka 15 kwa kikundi cha wageni ambao walishtakiwa kwa kuingia nchini na zaidi ya dola milioni tatu na nusu, kinyume na sheria, ili kuwalipa maharamia kikombozi.

Washtakiwa sita, kutoka Uingereza, Marekani na Kenya walikamatwa mwezi uliopita,punde baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege mjini Mogadishu.

Watu hao walifanyiwa kesi ya faragha kwenye uwanja wa ndege ambako walitua mwezi uliopita.

Inasemekana walipowasili Mogadishu walikuwa wamebeba mamilioni ya dola kama kikombozi.

Fedha hizo zimetaifishwa pamoja na ndege mbili walizopanda.

Msiamo rasmi wa serikali ya Somalia ni kuwa inapinga kulipa kikombozi lakini tabia hiyo imekuwa ni kawaida sasa.

Umoja wa mataifa unakisia zaidi ya dola milioni moja zililipwa kwa maharamia wa Somalia mwaka jana.

Haijulikani kwanini hao wanaume sita wakawa wamewakera wakuu.