Waziri Mkuu wa Somali ajiuzulu

Mohamed Abdullahi Mohamed Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Mohamed Abdullahi Mohamed

Waziri Mkuu wa Somalia, Mohamed Abdullahi Mohamed amejiuzulu kufwatana na mkataba ulioungwa mkono na Umoja wa Mataifa ili kumaliza msukosuko wa nchi hiyo.

Bwana Mohamed ambaye juma hili alisema hatoondoka amesema ameamua kung'atuka kwa sababu ya maslahi ya watu wa Somalia.

Maelfu ya wa Somali waliandamana kupinga uamuzi wa kumuondosha waziri mkuu wakisema kuwa anawalipa watu mishahara yao.

Pia, alipiga vita rushwa na amepiga hatua dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu ambao wanadhibiti sehemu kubwa ya nchi.