Chris Hughton kocha mpya Birmingham City

Chris Hughton amethibitishwa kuwa meneja wa Birmingham City, baada ya kukamilisha mkataba kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Alex McLeash.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Chris Hughton

Meneja huyo wa zamani wa Newcastle, hakuwa akijishughulisha na soka moja kwa moja tangu alipofukuzwa kazi na Newcastle mwezi Disemba.

Hughton aliipandisha daraja Newcastle, na mmiliki wa Birmingham Carson Yeoung anatarajia atafanya hivyo na City.

Inaaminika kuwa Hughton alipewa kipaumbele kuliko Roberto di Matteo kuchukua nafasi ya McLeaish.

Taarifa ya City imesema: "Kufuatia mazungumzo tuliyofanya, kaimu mwenyekiti Peter Pannu amehisi kuwa Hughton ndio anafaa.

"Pannu alipendezwa na mtazamo na mipango ya soka ya Houghton ya kujenga vijana na kucheza soka la kuvutia."

Klabu hiyo bado haijathibitisha mkataba wa Hughton utakuwa na muda gani, au nani atakuwa msaidizi wake.