Huwezi kusikiliza tena

Siku ya wajane duniani

Siku hii inaadhimishwa kwa mara ya kwanza duniani. June 23 imekuja kutokana na kampeni za mwanasiasa mmoja Muingereza ambae, alifiwa na baba yake akiwa mtoto nchini nchini India. Serikali ya Gabon ilidhamini azimio hilo la Umoja wa Mataifa.

Inakisiwa kuna takriban wajane millioni 245 duniani na 115millioni wanadhulumiwa wakikabiliwa na ukatili,umasikini na kutengwa na jamii.

Siku inayodhamira kutoa fursa ya kuzungumzia matatizo yanayowakumba wajane hasa wanawake na watoto wao ili kurejesha haki zao na kupambana na umaskini kwa kuwezeshwa.

Miongoni mwa matatizo yanayowakumba wajane ni pamoja na kunyimwa haki ya kurithi na haki ya kumiliki ardhi, na wengine hata hunyimwa haki ya kumzika mume wako.

Wajane hao wa kike wengine huondolewa kwenye nyumba zao na kupigwa, baadhi huuliwa na ndugu zao wenyewe.

Katika nchi nyingi, hadhi ya mwanamke inahusishwa zaidi na maisha yake na mumewe, na hivyo mume anapokufa, mwanamke anakuwa hana nafasi yeyote kwenye jamii.

Wengine hutakiwa kuolewa na ndugu wa mume wake bila ridhaa zao. Na huo ni mwanzo tu wa matatizo mengi yajayo.

Watoto wa wajane hao nao huathirika sana kisaikolojia na kiuchumi.

Wajane wengine hulazimika kuwatoa watoto wao shuleni, ukizingatia hana msaada wowote hivyo watoto kufanya kazi za kuinua maisha yao.

Wachangiaji katika mjadala huu ni

Bi Tuzie Muze- mjane aliyopo Dar es Salaam, Tanzania.

Bi Rosemary Nafula- mjane aliyopo Kenya

Bi Jane Magigita- mwanasheria kutoka kituo cha msaada wa sheria kwa wanawake, WILAC- Dar es Salaam

Judy Okal- wakili kutoka shirikisho la wanawake wanasheria nchini Kenya, FIDA