Haruna asajiliwa na Dynamo Kiev

Lukman Haruna Haki miliki ya picha Getty
Image caption Lukman Haruna

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Nigeria Lukman Haruna ametia saina mkataba na klabu ya Ukraine Dynamo Kiev.

Duru zinasema Klabu hiyo ilimsajili mchezaji huyo kwa kitita cha $2.8m kutoka kwa klabu ya AS Monaco ya Ufaransa.

Haruna alijiunga na Monaco mwaka wa 2007 muda mfupi baada ya kukiongozxa klabu ya Nigeria ya vijana wasiozidi umri wa miaka 17 kwenye fainali za kombe la dunia nchini Korea Kusini.

Mchezaji huyo alikuwa miongoni mwa kikosi cha timu yab taifa ya Nigeria, Super Eagles iliyoshiriki kwa fainali za kombe la dunia nchini Afrika Kusini na kilichochuana na Argentina na Ugiriki.

Klabu ya Monaco iliondolewa kutoka ligi kuu daraja ya kwanza Ufaransa mwaka huu.

Vilabu kadhaa vya Uingereza na Ufaransa vilikuwa vimeonyesha nia ya kumsajili mchezaji huyo lakini havikuweza kutoa fedha iliyoitishwa na klabu ya Monaco.