Imebadilishwa: 24 Juni, 2011 - Imetolewa 19:11 GMT

Video

Tanzania bado yadai fedha zake

Media Player

Unahitaji toleo sahihi la Flash Player kucheza sauti/video

Cheza katika media player

Sakata la kashfa ya uuzaji wa rada kwa Tanzania kutoka kampuni ya Uingereza- BAE Systems bado inaendelea, baada ya kampuni hiyo kusita kuilipa serikali ya Tanzania fedha hizo moja kwa moja serikalini na badala yake ilipe asasi za serikali za Uingereza. Kampuni hiyo inadai kutokana na sera zake hairuhusiwi kuilipa serikali na hivyo njia mbadala ni kupitia mashirika hayo.

Kampuni ya BAE imetakiwa kuilipa Tanzania fidia ya paundi milioni 29.5 baada ya kuiuzia Tanzania rada kwa gharama ya paundi milioni 41 za Uingereza wakati bei halisi ilikuwa paundi milioni 12.

Ujumbe wa wabunge watano wakiongozwa na naibu spika wa Tanzania Bw Job Ndugai wamefika nchini Uingereza kuishinikiza kampuni hiyo kuilipa serikali ya Tanzania. Mazungumzo mpaka sasa bado yanaendelea na yanaonekana kuwa na mwelekeo mzuri.

Mwandishi wa BBC Zuhura Yunus amefanya mahojiano na Bw Ndugai kujua zaidi kuhusu suala hilo.

BBC navigation

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.