Polisi wapambana na raia Misri

Maandamano Misri Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Maandamano Misri

Mamia ya jamaa wa Wamisri waliouwawa au kujeruhiwa wakati wa maandamano ya kumuondoa Rais Mubarak, wamepambana na polisi nje ya mahakama ambayo inafanya kesi ya waziri wa mambo ya ndani ya nchi wa zamani.

Waliyarushia mawe magari ya polisi baada ya kutangazwa kuwa kesi ya Habib al-Adli inaahirishwa hadi mwezi ujao.

Bwana Adli ameshtakiwa kwa kutoa amri kuwa waandamanaji waliokuwa wakipigania demokrasi wauwawe.

Rais Mubarak mwenyewe anatarajiwa kufikishwa mahakamani mwezi wa Agosti.