Sudan wakubaliana na waasi Kordofan

Makubaliano yameafikiwa kumaliza wiki kadhaa za ghasia mjini Kordofan, Sudan Kusini, ambapo majeshi ya kaskazini yameshutumiwa kwa mauaji ya kimbari.

Waasi waliopigana upande wa kusini wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyochukua muda mrefu nchini humo wanatarajiwa kuchanganywa kwenye jeshi la kaskazini au kunyang'anywa silaha.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Sudan Kusini

Kordofan kusini liko mpakani mwa Sudan Kusini, linalotarajiwa kuwa huru mwezi Julai.

Takriban watu 70,000 wamekimbia makazi yao, huku majeshi ya kaskazini yakishutumiwa kulipua maeneo waishio jamii ya Wanuba.

Makubaliano hayo, yaliyosimamiwa na Umoja wa Afrika, pia inalihusu jimbo jirani la Blue Nile, ambalo limekuwa na amani.

Nyaraka zilizotolewa zimesisitiza kunyang'anywa kwa silaha hizo zitafanywa bila kutumia nguvu.

Mwandishi wa BBC alisema, jaribio la kunyang'anya silaha linaonekana kuwa imechochea mapigano makali Kordofan Kusini.