Huwezi kusikiliza tena

Wabunge, posho na marupurupu

Mjadala huu unaangazia kwa kina - mishahara, posho, marupurupu na kodi kwa wabunge katika nchi za Afrika Mashariki na kati.

Washiriki wetu ni pamoja na:

Mbunge Johnstone Muthama kutoka Kenya. Yeye alianza kulipa kodi siku nyingi kabla ya katiba mpya kuanza kutumika.

Mbunge Zitto Kabwe kutoka Tanzania, yeye anapendekeza posho zifutwe, pia pamoja naye ni mbunge Juma Nkamia anayependekeza posho hizo zisiondolewe na ikiwezekana ziongezwe.

Mchambuzi wetu ni Ali Mutasa mwandishi habari wa masuala ya uchumi kutoka Uganda.

Mjadala huu umeendeshwa na Zawadi Machibya