Bahrain inazungumza na upinzani

Wakuu wa Bahrain wameanza mazungumzo na upinzani, baada ya miezi kadha ya maandamano dhidi ya serikali ambapo watu zaidi ya 30 waliuwawa.

Haki miliki ya picha AP

Mfalme Hamad, wa madhebnu ya Sunni, amesema maswala yote yanaweza kujadiliwa.

Kundi kubwa la upinzani la Bahrain, lenye Washia, ambao ndio wengi nchini humo, liliamua dakika ya mwisho kuhudhuria mazungumzo.

Na kuna Washia wengi ambao wanashikilia kuwa mazungumzo na serikali hayataleta faida kwa hali ilivo hivi sasa nchini.

Viti 35 tu kati ya 300 katika baraza hilo la mazungumzo, vimetengwa kwa ajili ya makundi ya upinzani, na mamia ya wafuasi wa upinzani wangali gerezani.

Washia wamekuwa wakilalamika kwa muda mrefu kwamba wanabaguliwa nchini Bahrain.

Waliandamana mwezi wa Februari, wakipata moyo kutoka maandamano ya Tunisia na Misri.