Ghasia mjini Karachi, Pakistan

Wanajeshi wa mgambo wa Pakistan wamedhibiti baadhi ya mitaa ya mji wa Karachi -- mji mkuu wa biashara nchini Pakistan -- ambako watu kama mia moja wameuwawa juma hili.

Siku ya Ijumaa, serikali ilitoa amri kwamba yeyote aliyehusika na ghasia hizo, apigwe risasi papo hapo.

Ghasia hizo zinahusishwa na magengi yenye silaha yanayoshirikiana na makundi ya kisiasa na kikabila, yanayopingana.

Magari ya kubeba majeruhi na magari ya deraya ya jeshi, sasa yanazihamisha familia, zilizonasa majumbani mwao kwa siku kadha, bila ya chakula wala maji.