NATO inazidisha mashambulio Libya

NATO inasema imezidisha mashambulio dhidi ya jeshi la Kanali Gaddafi, magharibi mwa Libya.

Haki miliki ya picha AFP

Jumuiya hiyo ya kijeshi, inasema ndege zake zimeshambulia zaidi ya sehemu 50 za kijeshi katika siku chache zilizopita, katika eneo la kutoka bandari ya Misrata, inayodhibitiwa na wapiganaji, hadi milima ya Nafusa, kama kilomita 90 nje ya mji mkuu, Tripoli.

Mapigano piya yanaendelea pembezoni mwa milima ya Nafusa baina ya wapiganaji wa Libya na wanajeshi wa Kanali Gaddafi.

Pande zote mbili zinajaribu kuania maeneo ya jangwa, ili kudhibiti njia muhimu za kuelekea mji mkuu.