Gaddafi anaweza kubaki Libya

Wapiganaji wa Libya wanasema Kanali Gaddafi anakaribishwa kubaki katika ardhi ya Libya , kama mstaafu; ikiwa atakubali nyendo zake kusimamiwa kimataifa.

Haki miliki ya picha BBC World Service

Kiongozi wa wapiganaji, Mustafa Abdel Jalil, alisema hayo alipozungumza na shirika la habari la Reuters mjini Benghazi.

Kanali Gaddafi ameshasema mara nyingi, kwamba daima hataondoka Libya; wakati wapiganaji na NATO wameshikilia kwamba mazungumzo ya amani hayawezi kufanywa, bila ya yeye kuacha madaraka.