Zuma anaongea na Urusi kuhusu Libya

Wizara ya Mashauri ya Nchi za Nje ya Afrika kusini inasema kuwa Rais Jacob Zuma anafanya ziara mjini Moscow, kama sehemu ya juhudi zake za kutafuta suluhu ya kisiasa katika vita vya Libya.

Haki miliki ya picha BBC World Service

Wizara hiyo imeeleza kuwa Bwana Zuma atahudhuria mkutano wa Ujumbe wa Kimataifa unaoshughulika na Libya, ambao unaijumuisha Urusi.

Urusi haikuthibitisha ziara hiyo.

Bwana Zuma anapatanisha kwa niaba ya AU katika mzozo wa Libya.