Gavana wa Hama, Syria, afukuzwa kazini

Rais Assad wa Syria amemtoa kazini gavana wa mji wa Hama, siku moja baada ya kufanywa maandamano makubwa mengine huko dhidi ya serikali yake.

Haki miliki ya picha AP

Kufukuzwa kwa gavana huyo kulitangazwa kwenye televisheni ya taifa.

Hapo jana iliarifiwa kuwa watu kama nusu milioni waliandamana katika mji wa Hama, bila ya kuzuwiliwa na askari wa usalama.

Mkaazi mmoja wa mji alisema Hama ni eneo lilokombolewa.

Mji huo ni kati ya mizizi ya maandamano nchini Syria, ambayo sasa yameendelea kwa miezi mine.