Vatikani inamkataa askofu wa Uchina

Vatikani imemtenga askofu ambaye alipewa hadhi hiyo na Uchina, bila ya kibali cha Papa.

Joseph Huang Bingzhang alivishwa uaskofu katika jimbo la Guangdong, siku ya Alkhamisi, na kanisa Katoliki linaloidhinishwa na serikali, na ambalo halitambui mamlaka ya Papa.

Katika taarifa kali, Vatikani piya ilisema kuwa Papa Benedict, analaani jinsi kanisa linavotendewa huko Uchina.

Uchina ina wakatoliki karibu milioni sita, ambao wamegawika baina ya kanisa linaloungwa mkono na chama cha kikoministi, na lile la chini kwa chini, tiifu kwa Papa.