Morocco wapiga kura mabadiliko ya Mfalme

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Mfalme wa Morocco Mohammed VI aliingia madarakani 1999

Wananchi wa Morocco wanapiga kura katika mfululizo wa mageuzi na mabadiliko ya kikatiba.

Mapendekezo hayo yaliletwa na Mfalme Mohammed VI na yanalenga kumpa waziri mkuu na bunge mamlaka zaidi.

Wachambuzi wanasema anatarajiwa kushinda japokuwa kujitokeza kwa wachache kunaweza kuamsha madai ya mabadiliko zaidi..

Mabadiliko yake yamechochewa na maandamano yanayoendelea katika nchi za kiarabu ambayo yaliyowaondoa madarakani marais wa Tunisia na Misri.

Vijana wa Morocco waliandaa vuguvugu lao kupitia mitandao ya kijamii mwezi Februari kwa wiki kadhaa kutaka kuwepo mabadiliko imbayo hatua iliyowafanya maelfu ya watu kuingia mitaani. Wamewataka wafuasi wao kususia kura hiyo.

"Tunakataa kilichopendekezwa. Bado kinawaacha vinara katika sehemu," mmoja wa waratibu wa vuguvugu hilo Najib Chawki aliliambia shirika la habari la Reuters

Baadhi wanaiita ‘siku kubwa ya maamuzi’ nchini Morocco. Hata hivyo wamorocco wanaonekana kuendelea na maisha yao ya kila siku bila vurugu yoyote ikilinganishwa na wakati wa rasimu ya mabadiliko. Baadhi ya watu wanasema in ukimya tu klabla ya mshindo mkuu.

Katika moja ya vituo vya kupigia kura katika eneo la Shule ya Hassan II katika mji mkuu Rabat, vyumba vyote vya kupigia kura vilikuwa sawa. Vina bendera ya Morocco na picha ya mfalme,

vyote vikiwavimewekwa pamoja katika ubao wa kufundishia. Ushiriki ulikuwa wa taratibu asubuhi lakini watu wanasema wengi watajitokeza baada ya swala ya Ijumaa.

Kuna dalili za matarajio katika ufalme, watu wengi wanahisi kuwa wanaandika historia na pia watu wanapiga kura kwa makini sana. Wanajua kuwa kura yao iwe –ndiyo au hapana- inaweza kuwakiliosha rasimu kwa mfalme mwenyewe.

Lakini vyama vyote vikuu vya upinzani, vyama vya wafanyakazi, vikundi vya kiraia na viongozi wa kidini na vyombo vya habari a kwa wiki kadhaa sasa vimekuwa vikiwataka wamorocco kupiga kura kuunga mkono katiba mpya.

Kura hiyo inayowakilisha rasimu ya mabadiliko ya kwanza ya katiba chini ya utawala wa mfame wa miaka 12, imeelezwa kuwa ‘tarehe ya kihistoria.’