Guterres azuru Dadaab

Mkuu wa wa Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amezuru kambi ya wakimbizi ya Dadaab nchini Kenya kujionea hali ilivyo.

Image caption Wakimbizi katika kambi ya Dadaab, kaskazini mwa Kenya

Hii ni wakati janga la ukame likizidi kuleta maafa nchini Somalia na maelfu kukimbilia nchi jirani ya Kenya.

Mkuu wa Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, alisema anataka mashirika ya kimataifa ya misaada yaende nchini Somalia ili kutatua tatizo la ukame mbaya nchini humo.

Katika mahojiano na BBC, Bw Guterres alisema Umoja wa Mataifa unajaribu kufika mikoa ambayo inadhibitiwa na kundi la wanamgambo la Al-Shabab.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Antonio Guterres

Alisema ukame uliopo Afrika Mashariki umeathiri vibya Somalia kuliko nchi nyingine katika ukanda huo.

Wasomali wengi walinaswa katika vita na hawawezi kufika katika kambi za wakimbizi katika nchi jirani za Ethiopia na Kenya, aliongeza.