Polisi kufutwa kazi Misri

Waziri Mkuu wa Misri ameamuru maafisa walioshutumiwa kwa mauji ya waandamanaji kufutwa kazi na kushtakiwa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Essam Sharaf

Waziri Mkuu wa Misri, Essam Sharaf, ameamuru kufutwa kazi kwa maafisa wote wa polisi walioshtumiwa kwa mauaji ya waandamanaji wakati wa vuguvugu za kumpinga Rais Mubaraka mwezi February.

Katika hotuba yake kupitia televisheni, Bw Sharaf alisema afisa yoyote anayetuhumiwa kuuwa raia atashtakiwa.

Alikuwa akizungumza na maelfu ya watu waliondelea na maandamano dhidi ya serikali yake katika eneo la kati kati mwa mji mkuu Cairo.

Waandamanaji wamekuwa wakidai hatua zichukuliwe dhidi ya maafisa wote wa polisi waliohusika na ghasia zilizosababisha mauaji ya watu takriban mia tisa.