Ombi la Liverpool lakataliwa na Villa

Klabu ya Aston Villa, imekataa ombi la Liverpool la kuitaka kumsajili mchezaji wake Stewart Downing kwa kitita cha £15m.

Image caption Stewart Downing mchezaji wa kiungo cha kati wa Aston Villa

BBC imegundua kuwa klabu ya Aston Villa, inataka kulipwa kitita cha £20m ili kukubali uuzaji wa mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Uingereza mwenye umri wa miaka 26.

Stewart ambaye alijiunga na Villa kutoka kwa klabu ya Middlesbrough kwa kitita cha £12m mwaka wa 2009, hajaafikiana na kocha wake Alex McLeish kuhusu kandarasi mpya na duru zinasema kuwa kocha huyo yuko tayari kumuuza stewart.

Mchezaji huyo wa kiungo cha kati pia amehusishwa na klabu ya Arsenal, lakini Liverpool ina nafasi nzuri ya Kumsajili.

Habari zaidi zinaendelea kujitokeza.