Ukosefu wa chakula Somalia ‘hauelezeki’

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watoto katika kambi ya wakimbizi Daadab, Kenya

Viwango cha utapiamlo kwa watoto wanaokimbia ukame Somalia kinaweza kusababisha ‘janga la kibinadamu ambalo haliwezi kufikirika’ , Mkuu wa shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema.

Watoto wadogo wanakufa njiani au wakti wamefika tu kwenye kambi Ethiopia na Kenya , UNHCR linasema.

Inakadiriwa kuwa robo ya Wasomali ama wamepoteza makazi yao ndani ya nchi au wanaishi nje kama wakimbizi.

Ukame mkali kutokea katika kipindi cha miaka 60 umechangia na pia vita ndani ya Somalia.

"Hailezeki, imepita kiasi," alisema msemaji wa UNHCR katika kitengo cha misaada Melissa Fleming. "wtu wetu wanasema hawajawahi kuona kitu kama kile."

Onyo hilo limekuja wakati mashirika ya misaada ya Uingereza Oxfam, Save the Children, na Msalaba Mwekundu yameanzisha kampeni ya maalum ili kushughulikia janga la njaa ambalo linawaathiri zaidi ya watu milioni 12 katika pembe ya Afrika.

Mashirika hayo kwa ujumla wake yanaomba karibu $150m (£93milioni).

UNHCR linasema mahitaji ya chakula, malazi, huduma za afya na misaada mingine muhimu ya kibinadamu ya dharura na kwa wingi.

Shirika hilo linasema zaidi ya asilimia 50 ya wtoto wa Kisomali wanaoingia Ethiopia wana hali mbaya kiafya kutokana na utapiamlo. Nchini Kenya idadi hiyo sawa na asilimia kati ya 30 na 40.

"Janga kubwa tunalolishuhudia, ni kuwa kuna watoto wanaowasili katika hali dhaifu sana, licha ya huduma ya dharura tunayowapa na matibabu ya chakula cha dharura, wanakufa ndani ya saa 24" Bi Fleming aliwaambia waandishi wa habari mjini Geneva.

"Tunakadiria kuwa robo ya Wasomali 7.5 milioni sasa ama wamepoteza makazi yao ndani yan nchi au wanaishi nje kama wakimbizi," alisema.

UNHCR hivi karibuni lilifungua kambi ya tatu Kusini Mashariki mwa Ethiopia mbayo inafikia uwezo wake wa kuchukua watu 20,000 unafikiwa kwa haraka na sasa ina mpango wa kuongeza kambi zingine.

Ndege ya misaada ya shirika la UNHCR ilielekea Addis Ababa Jumanne na ujumbe wa malori 20 yakiwa yamebeba mahema na misaada mingine ulielekea huko.

Kaskazini Mashariki nchini Kenya, kambi ya Daadab, kiasi cha wakimbizi 1,400 wanaingia kila siku. Mashrika ya misaada yana hofu kuwa idadi inaweza kupanda mpaka nusu milioni.

Badu Katelo, Kamishna wa Mausala ya Wakimbizi Kenya alisema ugawaji wa chakula na maji malzi na mahali, vyote vimewazidi uwezo na haliya usalama inazidi kuwa mbaya.

"Tungependa kuona jumuiya ya kimataifa inachangamka na kujitolea kuingilia kati ," alisema.

Mwansdishi wa BBC Ben Brown aliyeko katika kambi ya Daadab anasema vifo vya watoto wadogo vimepanda mara tatu zaidi huku watoto wengi walio chini ya umri wa miaka mitano wanakufa pindi wakifika tu au siku chahce baada ya kufika

Familia zinatembea siku nyingi bila chakula au maji kufika kambini, ansema mwandishi wa BBC, baadhi wakisema wanaibiwa njiani na kubakwa wakiwa njiani au kuvamiwa na wanyama.