Jamhuri ya Sudan ya kusini kuidhinishwa

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa litatoa mapendekezo ya kutaka Jamhuri ya Sudan ya Kusini itambuliwe kama mwanachama mpya wa Umoja wa Mataifa.

Haki miliki ya picha afp
Image caption Mwanachama wa 192

Kuna hisia za kuridhia ufanisi kwenye Umoja wa Mataifa, chombo kilichosimamia mapatano ya amani na kusababisha sehemu ya Kusini kujitenga kutoka Sudan.

Licha ya hisia za kufanikiwa bado kuna hali ya mashaka kuhusu majaliwa ya Taifa hili changa kutokana na mvutano wa hivi karibuni kwenye eneo la mpaka baina ya Kaskazini na Kusini.

Kuna hisia za mafanikio makubwa miongoni mwa wajumbe wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. Tangu mwaka 2005 Umoja wa Mataifa umechunguza mapatano yaliyowezesha kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe baina ya Kusini na Kaskazini, na kusimamia kura ya maoni iliyopelekea Uhuru wa eneo la Kusini.

Kwa hiyo kukubalika kama mwanachama mpya wa Umoja wa Mataifa itakuwa kama kutimiza wajibu, hatua itakayoanza kwa pendekezo kuwasilishwa mbele ya Baraza na kupitishwa siku ya pili kuwa Taifa la 192 la Umoja huo.

Hata hivyo wengi wana hofu juu ya majaliwa ya Taifa hili, kwa sababu katika majuma machache yaliyopita hofu ya kuzuka vita imejitokeza kuliko wakati wowote katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, juu ya eneo linalozozaniwa la Abyei.

Haki miliki ya picha unknown
Image caption Hali ni tete Abyei

Halikadhalika, Jeshi la Sudan linaeneza kampeni ya uhasama dhidi ya wapiganaji wa Kinubi walio kaskazini mwa mpaka, mzozo ambao unaweza kuivuta Sudan ya kusini kwa sababu Wanubi wamekuwa washirika wao.

Hapa Umoja wa Mataifa hautokuwa na ushawishi wowote, sababu Mamlaka yake huko Kaskazini yalitoweka kufuatia Uhuru wa eneo la Kusini.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Umoja wa Mataifa Sudan

Ingawaje wiki hii Baraza la Usalama lilipiga kura kutimiza wajibu ya kuweka vikosi vyake katika eneo hilo lenye mgogoro. Limeamuru vikosi vingine visaidie katika ujenzi wa miundo mbinu ya Sudan ya Kusini ili kulifanya liwe Taifa kamili. Na vilevile kuhifadhi amani huko Abyei, licha ya kuwepo masuala mengi ya kusluhisha, kila mshirika akifahamu vyema kuwa hali huko ni tete.