UN yalaani mashambulizi Mumbai

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mashambulizi ya Mumbai

Taarifa hiyo imesema ugaidi wa ina yoyote ile ni tisho kubwa kwa amani na usalama duniani. Wanachana wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani vikali kile wametaja kama mashambulio ya kigaidi yaliyolenga maeneo tofauti mjini Mumbai India hapo Jumanne.

Aidha wametoa rambirambi kwa jamaa za waathirika sawa na serikali ya India. Baraza la Usalama kwenye taarifa yake limesisitiza kwamba kitendo chochote kile cha ugaidi kinatishia amani na usalama wa dunia na kwamba vitendo hivyo ni vya jinai na havifai kwa vyovyote kukubaliwa kuendelea, pasina kujali maazimio ya wanaotekeleza.

Wanachama wa baraza hilo wameongeza kwamba wakati wote wako tayari kuzima aina zote za ugaidi kwa mujibu wa azimio la Umoja wa Mataifa.

Huku haya yakiarifiwa rais wa Marekani Barack Obama ameiambia India kuwa Marekani ilikuwa tayari kuwasaka waliohusika na mashambulio hayo huku serikali jirani ya Pakistan pia ikilaani matukio hayo. Mwaka 2008 zaidi ya watu mia moja waliuawa katika msiruru ya mabomu na mashambulizi ya kuvizia kutoka kwa watu waliokuwa na silaha mjini Mumbai ambapo walilenga hoteli mbili kuu za kifahari. Mwaka uliotangulia Mambomu yaliyotegwa ndani ya treni ya abiria yalilipuka na kuwaua karibu watu mia mbili na wengine wengi kujeruhiwa.

Kufuatia mashambulizi hayo na yale ya karibuni makundi ya wanamgambo yanayoendesha shughuli zao nchini Pakistan yameendelea kulaumiwa na India kwa kuhusika na mashambulizi ya kigaidi.