Njaa ya athiri maeneo zaidi Somalia

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa sehemu zingine tatu nchini Somalia zinakabiliwa na baa la njaa.

Kufikia sasa kuna maeneo tano nchini humo yanayokabiliwa na tatizo hili.

Baadhi ya sehemu hizo tatu zilikuwa maarufu sana kwa uzalishaji wa vyakula.

Sehemu hizo tatu mpya zinapatikana kusini mwa Somalia na karibu na mji mkuu wa Mogadishu.

Image caption Janga la njaa Somalia

Kati ya sehemu hizo tatu, Afgoye corridor ndio ilio na idadi kubwa zaidi ya watu ikiwa na urefu wa takrbani kilomita thelathini kwenye barabara kuu inayounganisha mji wa mogadishu na ule wa Afgoye.

Wakati somalia ilipokuwa nchi thabiti, mji huu wa Afgoye ulikuwa na shughuli nyingi wak

ati wa asubuhi, malori mengi yalikuwa yakisafirisha mboga na matunda hadi kwenye soko kuu mjini Mogadishu.

Nyakati za jioni, ili kuwa jambo la kawaida kuona idadi kubwa ya mifugo ikisafirishwa, kupitia mji huo hadi soka kuu la mifugo mjini Mogadishu.

Mwaka wa 2007, eneo hili liligeuka na kuwa makao ya zaidi ya watu nusu milioni waliokimbia mapigano mjini mogadishu kati ya wanajeshi wa ethiopia na wapiganaji wa waasi.

Tangu wakati huo mji wa Afgoye umekuwa kwa kiasi kikubwa kutokana na kuongezeka kwa nyumba za mabanda na zile za kifahari.

Eneo hili la Afgoye corridor limewavutia wafanyabiashara wengi, kampuni ya simu ya mkononi na kampuni kadhaa za uchukuzi zimefungua ofisi zao katika sehemu hii.

Kutokana na kuongezeka kwa shughuli nyingi katika eneo hili, sasa limekuwa mji mkubwa ambao raia wake wanapata huduma za kimsingi kama vile shule na hospitali.

Mji wa pili uliotangazwa kuwa unakabiliwa na baa la njaa ni mji wa Balad, ulioko kilomita 40 kaskazini mwa mogadishu.

Mto shabelle umepita katikati mwa mji huo na shughuli nyingi za kilimo zinaendelea viungani mwake.

Eneo hili lilikuwa likizalisha kiasi kikubwa cha pamba ndiposa kiwanda cha kutengeneza nguo kilijengwa mjini humo.

Na mji wa tatu ni ule wa Adale, mji mdogo ulioko pwani, kaskazini mwa mogadishu.

Mji huo una sehemu nyingi zenye ufuo mzuri na wakuvutia na ni maarufu kwa shughuli za uvuvi.

Miji hii mitatu kwa sasa inathibitiwa na kundi la la wapiganaji wakiislamu la al shabaab.