Kamanda wa Libya aliuliwa na wenzake

Viongozi wa wapiganaji wa Libya wanasema wafuasi wao wenyewe ndio waliomuuwa kamanda wa jeshi la wapiganaji hao, Jenerali Abdel Fattah Younes.

Haki miliki ya picha Reuters

Waziri wa Mafuta na Fedha wa wapiganaji, Ali Tarhouni, alisema Jenerali Younis aliuliwa na wapiganaji walioasi, na wanaoshirikiana na waislamu wenye msimamo mkali. Alisema haijulikani sababu yao ya kumuuwa kamanda huyo.

Alieleza kuwa waasi hao walimchukua Jenerali Younes na kumpiga risasi na kumuuwa, baada ya jenerali huyo kuitwa aende mbele ya kamati inayochunguza kama alikuwa mtiifu kwa wapiganaji.

Serikali ya Kanali Gaddafi ilisema mauaji hayo yanaonesha kuwa wapiganaji hawatoweza kuiongoza Libya, na hata wanashindwa kuwalinda viongozi wao.