Mchapishaji atozwa faini

Kampuni moja maarufu ya uchapishaji, Macmillan, imeamrishwa na mahakama kulipa kama dola milioni 18, kutokana na tuhuma wakala wake mmoja alitoa rushwa ili kupata kandarasi Afrika.

Haki miliki ya picha SPL

Tuhuma hizo kwanza zilitajwa na Benki ya Dunia ambayo iligharimia utaratibu wa kuchagua kandarasi, itayofaa kuziuzia vitabu shule za Sudan Kusini.

Idara ya Uingereza ya kupambana na ufisadi ilichunguza kisa hicho, na kuishtaki kampuni ya Macmillan.