Kikosi cha Nigeria chatajwa

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Nigeria ya vijana wasio zidi umri wa miaka 20 John Obuh, amewashirikisha wachezaji wengi walioshinda kombe la bara la Afrika kwa vijana chipukizi nchini Afrika Kusini kwa michuano ya kombe la dunia zitakazoandaliwa nchini Colombia.

Image caption Mchezaji wa timu ya taifa ya Nigeria

Noadha kwa timu hiyo Ramon Azeez na mfungaji bora wa mabao AYC Uche Nwofor ni miongoni mwa wachezaji hao 21 waliojumuishwa kwenye kikosi cha Fying Eagles.

Hata hivyo Onazi Ogenyi anayechezea klabu ya Lazio nchini Italia ameachwa nje kufuatia jeraha. Mlinda lango Jamiu Alimi anayechezea klabu ya Westerlo ya Ubelgiji pia ameachwa nje.

Wachezaji wengine walioachwa nje ni pamoja na Gbenga Arokoyo, Kelly Godwin na Chidi Osuchukwu.

Image caption John Obuh

Licha ya kutawala michuano mingi ya soka barani Afrika, Nigeria haijashinda kombe lolote la la vijana tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo mwaka wa 1979.

Timu hiyo ya Flying Eagles ilimaliza katika nafasi ya pili miaka wa 1989 na 2005, wakati waliposhindwa na Ureno na Argentina katika fainali mtawalia.

Nigeria imejumuishwa kwenye kundi la D pamoja na Guatemala, Croatia na Saudi Arabia.

Cameroon, Misri na Mali ni wawakilishi wengine wa bara la Afrika katika mashindano hayo ya dunia yatakayoanza tarehe 29 mwezi huu hadi tarehe 20 mwezi Agosti.