Gaidi wa Norway ni mwananchi

Polisi wa Norway wamemshtaki Anders Behring Brevik akituhumiwa kuhusika na mashambulio mawili yaliyotokea Ijumaa.

Haki miliki ya picha Reuters

Yale yanayojulikana kuhusu Brevik ni yale yaliyochapishwa katika tovuti za mawasiliano kama Twitter na Facebook - na haya yanaonesha yaliandikwa siku chache tu zilizopita.

Polisi wanasema maandishi yake kwenye mtandao wa internet, yanaonesha alikuwa na msimamo wa mrengo wa kulia na alikuwa dhidi ya Waislamu.

Kwenye Facebook alijielezea mwenyewe kuwa Mkristo na wa mrengo wa kulia.

Picha yake kwenye Facebook inaonesha mwanamme mwenye nywele za "blond" na macho ya buluu.

Inafikiriwa Bwana Brevik alikulia mjini Oslo.

Baadae alihama mjini na kuanzisha kampuni yake, iitwayo Brevik Geofarm.

Taarifa zinasema kampuni hiyo ilianzishwa ili kulima mboga.

Vyombo vya habari vya Norway vinafikiri alitumia kampuni hiyo kununua mbolea, ambayo inaweza kutumiwa kutengeneza mabomu.

Gazeti la Norway la Verdens Gang, linamnukuu rafiki yake akisema kuwa mshukiwa alipokuwa anakaribia mika 30, alibadilisha msimamo wake na kuwa na mawazo makali ya mrengo wa kulia.

Piya alishiriki katika tovuti zinazohusu msimamo mkali wa kizalendo.