Afisa wa Sudan Kusini auwawa

Kiongozi wa wapiganaji wa Sudan Kusini, ambaye alitia saini mkataba wa amani na serikali, ameuwawa katika hali ya kutatanisha.

Haki miliki ya picha AP

Wanachama wa kikundi cha Gatluak Gai wanasema afisa huyo aliingia katika mtego wa serikali na kuuwawa.

Serikali ya Sudan Kusini inasema aliuliwa na wafuasi wake.

Kanali Gai ni kutoka kabila la Nuer ambalo limekuwa likizozana na Wadinka, kabila kubwa kabisa katika serikali ya Sudan Kusini.

Mwandishi wa BBC alioko Sudan anasema mauaji hayo yatawafanya viongozi wengine wa wapiganaji, kusita kukubali msamaha unaotolewa na rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir.