Malema ashutumiwa kujilimbikizia mfuko

Gazeti moja la Afrika Kusini, limedai kuwa mwanasiasa maarufu, anayeongoza tawi la vijana la ANC, alitumia mfuko wa wakfu wa siri, kugharimia maisha yake ya anasa.

Image caption Julius Malema

Gazeti hilo, City Press, linadai kuwa, Julius Malema, alipata malipo kutoka wafanyabiashara, ili kuwasaidia kupata kandarasi za serikali.

Bwana Malema alikanusha kuwa mfuko unatumiwa kupitisha na kusafisha fedha.

Msemaji wake hakupatikana kutoa maelezo.

Bwana Malema ni mtu anayezusha utatanishi, na wadadisi wanasema, huenda kauli yake ikawa muhimu kwa kiongozi ajaye wa ANC.