Niko tayari kueleza sababu zangu-Breivik

Wakili anayemuakilisha mshukiwa mmoja mwenye umri wa miaka 32, Anders Behring Breivik,raia wa Norway, ambaye anakabiliwa na mashtaka kuhusiana na mauaji ya vijana katika kambi moja na shambulio la bomu mjini Oslo, siku ya Ijumaa, amesema mteja wake amekiri kutekeleza mashambulio hayo akitaja vitendo vyake kama vya kikatili lakini vilivyohitajika.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Anders Behring Breivik

Wakili wa Breivik, Geir Lippestad, amesema mshukiwa huyo yuko tayari kuelezea mbele ya mahakama sababu zilizompelekea kufanya vitendo kama hivyo siku ya juma tatu.

Watu 85 wamethibitisha kuuawa wakati mshukiwa huyo alipowafyatulia risasi kiholela vijana waliokuwa wakihudhuria mkutano wa chama tawala cha Leba katika kisiwa cha Utoya.

Awali watu wengi saba waliuawa kwenye shambulio la bomu kati kati mwa Oslo.