Njaa Pembe ya Afrika: Ufaransa yatahadharisha kuwa 'kashfa’

Image caption Watoto wakipatiwa msaada wa chakula Mogadishu

Dunia ‘imeshindwa kuhakikisha kuna chakula cha kutosha’, Waziri wa Kilimo wa Ufaransa amesema katika mkutano msaada wa chakula.

Mkutano huo ni wa Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Chakula unaojadili ukame katika eneo la Mashariki na Pembe ya Afrika.

"Kama hatutachukua hatua madhubuti, njaa itakuwa kashfa ya karne hii." Shirika la Habari za AFP limemnukuu Bruno Le Maire akizungumza mjini Rome.

Zaidi ya watu milioni 10 inakadiriwa kuwa wako katika hali ya hatari ya ukosefu mkubwa wa chakula na baa la njaa limetangazwa katika maeneo mawili nchini Somalia.

Mbele ya mkutano huo, Benki ya Dunia imeahidi msaada wa dola milioni 500 (£307milioni).

Kiasi cha dola 12milioni kitapelekwa mara moja kusaidia waloathirika zaidi na kile Umoja wa Mataifa unakiita Ukame mbaya zaidi kutokea eneo la Afrika ya Mashariki katika miaka 60.

Lakini kiasi kikubwa cha fedha kitaelekezwa katika miradi ya muda mrefu ya kuwasaidia wakulima na pia wafugaji.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito kwa mataifa wafadhili kutoa pesa zaidi za msaada kiasi cha dola 1.6

Awali shirika la Msalaba Mwekundu limesema limegawa chakula katika maeneo yaliyoathirika zaidi yanayodhibitiwa na makundi ya wapiganaji wa kiislam.

Wakifanya kazi kwa kupitia kamati ya wenyeji, Shirika la Msalaba Mwekundu limegawa chakula kwa watu 24,000 kwa lori.

Kuna mashirika mengi ya misaada ya ndani ambayo tayari yanafanya kazi nchini kote Somalia-ukweli kwamba mara nyingi unapotelea kwenye usumbufu wa al-Shabaab juu ya mtazamo wa kikatili unaoelekezwa kwa mashirika makubwa WFP.

Hakuna mashaka kuwa ukame, na harakati za mageuzi kwa nchi za Kiarabu yametikisa hali ya usalama nchini Somalia.

Ushahidi usiothibitishwa unaonyesha kuwa al-Shabab sasa wameishiwa fedha, wamegawanyika zaidi na wapiganaji wengi wa jihadi kutoka nje waliokuja kujiunga nao wameondoka kwenda kujiunga na makundi mengine.

Al-Shabab, kundi linalohusishwa na al-Qaeda linadhibiti sehemu kubwa ya maeneo ya Kusini na Kati nchini Somalia, liliweka amri ya kuzuia mashirika ya misaada ya kigeni katika maeneo yake mwaka 2009, katika kwa sasa limeruhusu kwa sehemu misaada itolewe.

Lakini WFP linasema bado haliwezi kuwafikia watu wapatao milioni 2.2 ndani ya Somalia huku wakimbizi wakiendelea kumiminika kwenye mipaka ya nchi za Kenya na Ethiopia.

Somalia inaripotiwa kuathirika zaidi na upungufu mkubwa wa chakula, lakini Kenya na Ethiopia pia zimeathiriwa.

Wachambuzi wanasema ukame umesababishwa na upungufu wa mvua na kushindwa kwa serikali kuiwesha miradi ya kilimo na umwagiliaji kifedha

Mkutano wa mawaziri kutoka mataifa ya G20 katika makao makuu ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa mjini Roma liliombwa na Ufaransa, mwenyekiti wa sasa wa Kundi la G20 lenye nguvu Kiuchumi.

"Mkutano wetu ni suala la kufa na kupona kwa makumi ya maelfu ya watu ," Bw Le Maire alisema wakati mkutano huo ulipofunguliwa, kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Habari la AFP.

Bob Geldof na wanaharakati wengine mashuhuri wanatoia wito kwa jumuiya ya kimataifa kutoa pesa zaidi za msaada.

Wanazishutumu nchi kama Italia, Ufaransa, Mataifa ya Kiarabu na Ujerumani kuwa kuchangia kidogo sana ikilinganishwa na utajiri zilizo nao.

Bw Le Maire ameimbia BBC kuwa lengo la mkutano huo lilikuwa ni kuratibu msaada na kukabiliana na baa hilo.

"Lengo la pili ni kutafakari kuhusu za siku za usoni na mtazamo wa muda mrefu kwa sababu tunachokiona Afrika ni kwamba watu wanahitaji kuwa a chakula chao wenyewe na kuwa na kilimo chao" alisema.

Mchambuzi wa BBC Afrika Martin Plaut anasema watu wengi walio katiakti mwa janga hili huko Ethiopia wamejitokeza lakini hawajasikiwa.

Hii ni kutokana na serikali ya Addis Ababa ina mpango kamambe wa kuchukua tahadhari, anasema.

Kujipanga mapema kwa tahadhari kuna maana kuwa utawala Ethiopia unaweza kuidhibiti mapema mara noja ukame unapojitokeza zaidi.

Ugawaji wa chakula wa kwanza ulianza mwezi February na umeendelea katika maeneo yaliyoathirika zaidi katika ukanda huo.

Jamii zinapata shida, lakini njaa iliyoikumba nchi jirani ya Somalia, Ethiopia wameiepuka na mfumo wa kudhibiti majanga uliowengwa tangu mwaka 1980s umefanya kazi.