Batista aondolewa ukocha wa Argentina

Sergio Batista amekubali kuacha ukocha wa timu ya taifa ya Argentina baada ya nchi hiyo kutolewa hatua ya robo fainali ya kuwania kombe la Copa America.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Sergio Batista

Wenyeji Argentina walitolewa na mabingwa Uruguay kwa mikwaju ya penalti.

Batista, mwenye umri wa miaka 48, amekuwa akiifundisha Argentina kwa mwaka mmoja sasa, awali akiwa kocha wa muda, baada ya Diego Maradona kutimuliwa kufuatia kutolewa katika Kombe la Dunia mwaka 2010.

Msemaji wa Chama cha Soka cha Argentina (AFA) amesema Batista hajatimuliwa, lakini imeamuliwa "kutengua" mkataba wake.

Argentina, ambayo mara ya mwisho kunyakua kombe muhimu ilikuwa mwaka 1993 waliposhinda mashindano ya Copa America, wamefuta mechi ya kirafiki dhidhi ya Romania mjini Bucharest iliyopangwa kuchezwa tarehe 10 mwezi wa Agosti.

"Makocha wa Argentina kwa viwango vyote wanafanyiwa tathmini na tume ta makocha wa taifa," aliongeza Bialo.

"Hakuna muda maalum uliowekwa, hakuna sababu ya kuharakisha kumchagua kocha mpya, kwa hiyo kuna mchakato wa kuwasoma na kuwafikiria makocha."