Beckham amtetea Balotelli kwa mbwembwe

David Beckham amemtetea Mario Balotelli kutokana na utata uliojitokea wakati akiwa karibu na lango alipoupiga mpira kwa kisigino badala ya kufunga, hali iliyomsabababishia atolewa nje na meneja wake wakati Manchester City ilipopambana na LA Galaxy.

Haki miliki ya picha Other
Image caption Mario Balotelli

Meneja wa Manchester City Roberto Mancini alihoji umahiri wa mchezaji huyo baada ya makusudi kukataa kufunga bao la wazi.

"Niliangalia tena, kutokana na tabia yake, naamini alidhani alikuwa ameotea," alisema Beckham, huku akimshauri Balotelli aendelee kufunga katika mechi zijazo.

"Mario amekuwa mchezaji hodari kwa miaka michache iliyopita na bado ni kijana mdogo sana."

Nahodha huyo wa zamani wa England, ambaye aliwahi kuichezea Manchester United ambao ni mahasimu wakubwa wa Manchester City, ameongeza: "Ataendelea kurjirekebisha, nina hakika.

"Lakini iwapo unadhani umeotea au la, hiyo haina maana. Kuna vijana wengi wadogo wanaziangalia hizi timu na wachezaji nyota waliokuja hapa.. Ni lazima uoneshe umahiri wako an ufunge bao."

Mancini, ambaye alizozana na Balotelli wakati akitoka uwanjani baada ya dakika 31, amesisitiza mshambuliaji huyo alipokuwa Inter Milan na yeye akiwa meneja wake alijua hakuwa ameotea.

"Katika soka kila wakati unatakiwa kuonesha umahiri, kila wakati unakuwa makini na kwa wakati ule hakuwa makini na hakuonesha umahiri wake," alisema.