Watu 11 wauwawa katika ghasia Uchina

Xinjiang China
Image caption Xinjiang China

Vyombo vya habari vya Uchina vinasema kuwa watu 11 wameuwawa katika kisa cha pili cha ghasia katika majuma mawili, kwenye jimbo la magharibi la Xinjiang.

Shirika la habari la taifa, Xinhua, lilisema watu wanane walikufa jana usiku katika mji wa Kashgar, wakati wanaume wawili walipoliteka lori na kuwapiga visu wapita njia.

Kabla ya shambulio hilo, kulitokea miripuko miwili.

Xinhua imeripoti kuwa leo piya kulitokea mripuko mwengine, uliouwa watu watatu.

Kulitokea ghasia za kikabila katika jimbo la Xinjiang, miaka miwili iliyopita, kati ya watu wa kabila la Uighur, ambao ni Waislamu, na ni wachache, na wanachukia utawala wa Beijing.

Wa-Uighur wanaoishi uhamishoni, wanasema kulikuwa na amri ya kafyu huko Kashgar, na watu kama mia-moja wamekamatwa.