Jenson Button amshinda Vettel Hungary

Jenson Button wa timu ya McLaren amefanikiwa kushinda mbio za langalanga za kusisimua za Hungary Grand Prix, huku mbio hizo zikiathiriwa kwa kiasi fulani na hali ya hewa ya mvua.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jenson Button

Button aliweka magurudumu mapya akisimama kwa mara ya tatu kabla mvua kuanza kunyesha na akafanikiwa kumpita mwenzake wa timu moja Lewis Hamilton na akafanikiwa kuongoza.

Hamilton aliyeshika nafasi ya nne , alisimama mara sita lakini aliweza kumpita Mark Webber wa timu ya Red Bull.

Kinara wa timu ya Red Bull Sebastian Vettel alimaliza katika nafasi ya pili huku Fernandom Alonso wa timu ya Ferrari alikuwa wa tatu.

Button amekamilisha mbio zake mara ya 200 na kuweka rekodi ya kushinda mara ya pili nchini Hungary, ambapo miaka sita iliyopita alishinda kwa mara ya kwanza.

Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 31 anakuwa binadamu wa kwanza kushinda mbio hizo katika hali unyevunyevu, yakiwa mashindano ya pili kukabiliwa na mvua tangu yalipoanza mwaka 1986.

Vettel alijirekebisha kutonana na makosa ya mwanzoni na hatimaye akafanikiwa kushika nafasi ya pili, ambapo yeye alisimama mara tatu kubadilisha magurudumu.

Button alikuwa nyuma ya Hamilton aliyempita na kuongoza katika duru ya pili ya mbio hizo baada ya kumpita Vettel katika duru ya kwanza. Lakini wakati Hamilton alipoamua kusimama kubadili magurudumu akiwa amesimama mara yake ya tatu, Button alifuata mfano wa Webber na akaamua kuweka matairi ya mwanzo.

Uamuzi huo ulikuwa muhimu na wa maana wakati mvua ilipoanza kunyesha baada ya mizunguko 20 na baadae madereva wawili wa timu ya McLaren wakiongoza mara kadha kabla Hamilton kuanza kurudi nyuma kwa ajili ya kubadili matairi na Button akaitumia nafasi hiyo kuongeza wigo na kushinda.