Umoja wa Afrika kujadili Somalia

Somalia ukame Haki miliki ya picha AFP
Image caption Somalia ukame

Umoja wa Afrika umetangaza kuwa utafanya mkutano wa viongozi ili kuchanga msaada kwa watu wa Somalia walioathirika na ukame.

Taarifa hiyo imetolewa baada ya malamiko kadha katika vyombo vya habari vya Afrika, kwamba viongozi wa Afrika wameshindwa kuwasaidia Wasomali wanaokabili njaa.

Makamo Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Bwana Mwencha alitoa tangazo la mkutano, wakati akizuru kikosi cha usalama cha umoja huo mjini Mogadishu.

Umoja wa Mataifa unasema watu milioni 12 wanahitaji msaada wa haraka katika eneo hilo.